KARIBUNI MCHICHANI

Kwa Habari moto moto Kuhusu Siasa , Uchumi, Maisha, Elimu Na Mengine Mengi.



Wednesday, September 22, 2010

Kijana avunja rekodi kwa uzazi holela UK

Macdonald
LONDON, Uingereza
KIJANA mwenye umri wa miaka 25, ameweka historia Uingereza kwa kuzaa watoto 15 na wanawake 14, na baadaye kuwatelekeza. Taarifa zilisema kijana huyo Keith Macdonald,
 ambaye
mara kadhaa amewahi kufungwa jela kwa uhalifu, pia ametajwa kuigharimu serikali matunzo ya watoto wake hao. Kwa mujibu wa taarifa Macdonald ambaye ameelezwa ni mlevi na mcheza kamali, baadhi ya wazazi wenzake hao amekuwa akiwapata kwenye vituo vya basi na sehemu za starehe. Macdonald ameelezwa kuigharimu serikali jumla ya pauni za Uingereza milioni 1.5 (zaidi ya sh. bilioni 3.3) kwa mwaka, kwa ajili fedha za kujikimu na nyumba. Serikali imekuwa ikitumia fedha za walipa kodi, kuwasadia wasiojiweza, ambapo kila mzazi wa mtoto amekuwa akipewa posho ya kujikimu ya pauni 30,000 (sh. 66,900,000) kwa mwezi na posho ya nyumba ya pauni 50,000 (sh. 111,500,000). Kiwango hicho hakijumuishi gharama za elimu, matibabu na huduma zingine za umma kama usafiri. Macdonalad ambaye baadhi ya watu wametaka afungwe kizazi, ametajwa ni baba aliyeshika nafasi ya juu kwa kutowajibika kwa watoto wake. Taarifa zingine kutoka kwa mmoja wa wazazi wenzake zilidai kuwa Macdonald, ana wanawake wengine wawili aliozaa nao ambao bado hawajajitokeza. Kwa mujibu wa taarifa toka kwa wanawake zake. Zilidai kuwa alianza mambo ya uzinzi akiwa na umri wa miaka 10, na alikuwa akikataa kuvaa kondomu, na taarifa zingine zilidai ana wanawake zaidi ya 40. Taarifa zilisema alianza kuitwa baba alipokuwa na umri wa miaka 15, baada ya kupata mtoto wa kike na msichana Michelle Purvis ambaye sasa ana umri wa miaka 32

No comments:

Post a Comment