Mshiriki wa shindano la Big Brother kutoka Tanzania, Mwisho Mwampamba akiwa an rafiki yake Uti kutoka Nigeria.
Mshiriki wa shindano la Big Brother kutoka Tanzania, Mwisho Mwampamba, amenusurika
kutolewa katika jumba hilo, ambalo juzi Jumapili lilishuhudua mwanadada wa Zambia, Paloma, akitupwa Zizizini
Kwa mujibu wa kanuni mpya ya shindano hilo mwaka huu, washiriki wakitolewa kwenye Jumba la Big Brother, hupelekwa kwenye Zizi, ambako wanaishi pamoja na wanyama walio hai kama ng'ombe na kuku.

Mtangazaji wa shoo wa kutolewa kwa washiriki kwenye jumba hiloMshiriki wa shindano la Big Brother kutoka Tanzania, Mwisho Mwampamba akiwa an rafiki yake Uti kutoka Nigeria., IK, alisema juzi kuwa baada ya wiki tatu zijazo, washiriki "angalau wawili watarejeshwa kwenye nyumba kuu" katika kuthibitisha kauli kwamba hata washiriki waliopelekwa zizini bado wamo mchezoni na wanayo nafasi ya kutwaa zawadi ya kwanza ambayo ni dola 200,000 (sawa na Sh. Milioni 295 za Tanzania).

Munya amethibitisha kuwa anapendwa sana na Waafrika ambao ndio hupiga kura kwa njia ya simu na internet, baada ya kunusurika mara sita, ambapo kila aliyewekwa na kijana huyo kwenye 'chekeche,' alitupwa nje.
Hali hiyo ilimfanya mshiriki kutoka Ethiopia, Yacob, kumuita Munya kuwa "Bingwa Mtetezi" wakati walipowekwa pamoja kwenye chekeche.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment