KARIBUNI MCHICHANI

Kwa Habari moto moto Kuhusu Siasa , Uchumi, Maisha, Elimu Na Mengine Mengi.



Saturday, September 11, 2010

HISTORIA YA MIAKA 15 YA MISS TANZANIA.

                                                                              1994: Mrembo Aina Linda W. Maeda
Mara baada ya kushinda taji hilo na kumaliza mwaka wake mmoja wa kazi za jamii, alipata ofa mbalimbali za kufanya kazi za mitindo nchini Afrika ya Kusini, na hatimaye kuhamia huko na kuishi huko kwa karibu miaka 10 ambapo aliweza kupata marafiki wa jinsia mbalimbali na kutokana
na marafiki hao aliweza kupata mchumba Bwana Jean P. Guyeu, raia wa Ufaransa aliyekuwa akifanya kazi zake nchini Afrika ya Kusini. Mrembo huyo akiwa na mchumba wake huyo hatimaye walikuja nyumbani nchini Tanzania kufunga ndoa ambayo ilihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo wajumbe wa Kamati ya Miss Tanzania . Kamati inayoendesha Mashindano ya urembo nchini iliyomuwezesha kumfikisha hapo alipo mrembo Aina Maeda. Kwa sasa mrembo Aina na mume wake wanaishi jijini Cape Town, Afrika ya Kusini.

1995: Mrembo Emily Adolf









Baada ya kuanzishwa kwa Mashindano ya urembo nchini mwaka 1994 yaliendelea kufanyika mfululizo na mwaka 1995 yalipanuka zaidi na kupata Wawakilishi kutoka mikoani, na Mshindi kwa mwaka 1995 alikuwa Emily Adolf mwanafunzi wa Kidato cha pili shule ya Sekondari ya Central akitokea Makao Makuu Dodoma, ushindi ambao ulileta malumbano hadi Mrembo huyo ilibidi afukuzwe shule kwa madai ya kushiriki Mashindano hayo akiwa ni mwanafunz
Wanaharakati wa kutetea Haki za Wanawake nao walikuja juu na kupinga vikali kuanzishwa kwa Mashindano hayo, huku Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA wakiwa wamelivalia njuga suala hilo , pamoja na Taasisi mbalimbali za Dini zikipinga vikali suala la warembo hao kupita jukwaani huku wakiwa wamevalia Vichupi, [swimming costume au Bikini ]
Baadaye mwaka huo huo Baraza la Sanaa la Taifa ilibidi kuweka Kanuni na Taratibu za kuendesha Mashindano hayo na kuzuia vazi hilo la vichupi, pamoja na wanafunzi wote wa shule za Msingi na Sekondari kutoshiriki Mashindano hayo.
Mrembo Emily Adolf [Pichani] aliwakilisha Nchi pia katika Mashindano ya Urembo ya Dunia na aliporejea, Kamati ya Miss Tanzania kwa kushirikiana Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete wakati huo akiwa Waziri katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akishirikiana na Waziri wa Elimu wa wakati huo waliweza kumuombea nafasi ya kumaliza masomo yake mrembo huyo katika shule ya Sekondari ya Makongo.
Baadaye jamii ya Watanzania walianza kuelewa taratibu lengo na madhumuni ya Mashindano haya kwamba siyo kuwadhalilisha wasichana bali ni Mashindano ambayo yalikuwa yakiwapatia zawadi mbalimbali warembo hao ikiwa ni pamoja na ajira. Kwani wasichana wengi ambao walikuwa wakishiriki Mashindano haya pamoja na zawadi ya pesa taslimu na vitu mbalimbali pia walikuwa wakipata ajira mbalimbali kutoka kwa Wadhamini wa Mashindano hayo pamoja na wadau wengine ambao walikuwa wakiyafuatilia kwa karibu Mashindano hayo.
Mrembo Emily Adolf : Kwa sasa anamiliki Mgahawa mmoja hapa jijini uitwao Rumors Pub na pia ameolewa.




1996: Baada ya kupanuka kwa Mashindano ya urembo nchini, mwaka 1996 mrembo Shose Sinare alishinda taji la taifa
Mrembo Shose Sinare alikuwa akitokea mkoa wa Arusha na aliweza kuwakilisha nchi yetu katika Mashindano ya urembo ya dunia yaliyofanyika nchini India . Mrembo Shose alikuwa mrembo wa kwanza kutoka katika nchi za Afrika aliyeweza kuitisha mkutano na Waandishi wa Habari wa kimataifa wakati wa shindano hilo la urembo la dunia na kuelezea jinsi washiriki kutoka nchi za Afrika walivyokuwa wakibaguliwa.


Baada ya kurejea nchini na kumaliza muda wake wa mwaka mmoja wa kazi za jamii, mrembo Shose Sinare alipata nafasi ya kufanya kazi za Mitindo [Modeling] nchini Italy kwa muda mrefu na hatimaye kujipatia mchumba raia wa Italy na kufunga naye ndoa.


                                                                   1997: Mrembo Saida Kessy kutoka mkoa wa Arusha


1997: Warembo kutoka mikoani walionekana kushika chati, kwani mwaka uliofuata [1997] Mrembo Saida Kessy kutoka mkoa wa Arusha aliweza kushinda taji la Miss Tanzania na kuwakilisha nchi yetu katika Mashindano ya urembo ya dunia. Mrembo Saida Kessy kama warembo wengine waliomtangulia hawakuweza kushika nafasi yeyote ya juu, na aliporudi nchini aliendelea kufanya kazi za jamii kwa kipindi cha mwaka mmoja akiwa kama mrembo wa taifa, na pia aliweza kupata ofa mbalimbali za kazi ya uanamitindo.


Mrembo Saida Kessy aliyezaliwa mwaka 1975 kwa sasa anafanya kazi katika Mahakama ya Kimataifa ICTR iliyopo Arusha, ameolewa na pia ana mtoto mmoja.




1998: Mrembo Basila Mwanukuzi Mrembo kutoka Wilaya ya Kinondoni




1998: Mwaka huu ilikuwa ni zamu ya warembo kutoka mkoa wa D'salaam kwani waliweza kushika nafasi zote tatu za juu. Mrembo Basila Mwanukuzi Mrembo kutoka Wilaya ya Kinondoni, ndiye aliyeshinda taji la Miss Tanzania akifuatiwa na mrembo Nuru Doto Butamu pamoja na Diana Muhere. Mrembo Basila Mwanukuzi aliyezaliwa tarehe14/6/1978 .. pia aliweza kuwakilisha nchi katika Mashindano ya urembo ya dunia. Aliporejea na kumaliza mwaka mmoja wa kazi za jamii aliweza kupata ofa mbalimbali za kazi za Mitindo nchini Marekani ambapo aliishi huko kwa muda na kurejea nchini na kufanya kazi na Kampuni ya Multichoice, na baadaye kuajiriwa na Shirika la Umoja na Mataifa. Mrembo Basila Mwanukuzi, amefanya kazi na UNDP jijini Pretoria Afrika ya Kusini, na baadaye alihamia Addiss Ababa Ethiopia , kwa sasa yupo jijini D'salaam akiendesha biashara yake binafsi ijulikanalo kama The Look Beauty Parlor [Unisex]
 
 
1999: Mrembo Hoyce Temu
1999: Mrembo Hoyce Temu aliyezaliwa tarehe 20 Machi 1978 akitokea Wilaya ya Ilala jijini D'salaam ndiye aliyeshinda taji la Miss Tanzania na kuwakilisha nchi katika Mashindano ya urembo ya dunia yaliyofanyika nchini Uingereza mwaka huo. Mrembo Hoyce Temu anajulikana zaidi kama Mrembo wa Karne, hasa ushindi wake ulikuja wakati dunia ikitoka karne ya 20 na kuingia karne ya 21. Mrembo Hoyce Temu ambaye alifahamika zaidi kama Mrembo wa Millenium.


“ Miss Millennium 1999” ni mrembo aliyeiletea sifa sana Kamati ya Miss Tanzania na nchi kwa ujumla kwa kufanya kazi nyingi za jamii hata alipomaliza muda wake wa mwaka mmoja, mrembo Hoyce Temu ameendelea kufanya kazi za jamii hadi hivi sasa kwa kutumia jina la Miss Tanzania 1999.
Mrembo Hoyce Temu pamoja na kazi mbalimbali za Mitindo alizokuwa akizifanya pia alifanya kazi ya kuhamasisha kuchangia mfuko wa chakula kwa nchi maskini uliokuwa ukijulikana kama WFP Telefood. Baada ya kumaliza mwaka wake mmoja wa shughuli za jamii Mrembo Hoyce Temu alihamia nchini Marekani ambapo pamoja na shughuli zingine alizokuwa akizifanya pia alikuwa akisomea Shahada ya Juu ya Sheria katika Chuo cha Ohio nchini Marekani.
Kwa sasa yupo nchini akifanya shughuli binafsi za Ushauri [Consultancy]




2000: mrembo Jacqueline Ntuyabaliwe kutoka Wilaya ya Ilala
2000: Warembo wa jiji la D'Salaam waliendelea kushinda Taji la Miss Tanzania na mrembo Jacqueline Ntuyabaliwe kutoka Wilaya ya Ilala ndiye aliyeshinda taji la Mrembo wa Taifa kwa mwaka huo. Mrembo Jacqueline Ntuyabaliwe kama ilivyokuwa kwa warembo wengine aliwakilisha nchi katika Mashindano ya urembo ya dunia na aliporejea aliendelea kulitumikia taifa kwa kufanya kazi za jamii kwa kipindi cha mwaka mmoja.


Mrembo Jacqueline aliyezaliwa tarehe 6 Desemba 1978 kabla ya kushiriki Mashindano ya urembo alikuwa ni msanii wa muziki ambaye alikuwa akiimba na bendi iliyokuwa ikijulikana kama The Tanzanite. Kushinda kwake taji la Miss Tanzania kulimuongezea Hadhi na jina lake kufahamika zaidi na hatimaye kuendeleza fani yake ya muziki kama Msanii wa Bongo Fleva anayejitegemea. Hadi sasa hivi ameshatoa albamu kadhaa na pia amekuwa akitumbuiza katika maonyesho mbalimbali na katika Mashindano ya urembo ya Miss Tanzania .




2001: Mrembo Happiness Magese
2001: Kama kuna mwaka ambao kidogo mrembo wa Taifa Miss Tanzania aliweza kutingisha katika Mashindano ya urembo ya dunia ulikuwa mwaka 2001 ambapo Mrembo Happiness Magese akitokea Wilaya ya Temeke alishinda Taji la Miss Tanzania na kuiwakilisha nchi katika Mashindano ya urembo ya dunia yaliyofanyika nchini Afrika ya Kusini mwaka huo.


Mrembo Happiness Magese mwenye vipimo vya urefu 5'79” alikuwa ni mrembo aliyetingisha warembo wote waliotokea bara la Afrika, na hata Mrembo wa dunia aliyeshinda katika mwaka huo Mnigeria Agbani Darego alikiri mbele ya Vyombo vya Habari kwamba mrembo Happiness Magese kutoka Tanzania ndiye aliyekuwa tishio kwake.
Mrembo Happiness Magese aliyezaliwa tarehe 22 Septemba 1982 mara baada ya kumaliza mwaka wake mmoja wa kazi za jamii hakukaa nchini alichukuliwa na Kampuni ya Elite Fashions inayofanya kazi za Mitindo huko Afrika ya Kusini na kuzunguka nchi mbalimbali akifanya kazi mbalimbali za mitindo. Hadi hivi mrembo huyo bado yupo nchini huko kwa shughuli hizo.


 
 
                                                                                      2002: Mrembo Angela Damas
2002: Warembo wa Jiji la D'salaam waliendelea kushika chati kwa kutwaa Taji la Miss Tanzania , Mrembo Angela Damas kutoka Wilaya ya Ilala aliweza kushinda taji la Mrembo wa Taifa kwa mwaka 2002. Mrembo Angela Damas aliyezaliwa tarehe


16 Februari 1982. kama ilivyo kwa warembo wengine, aliwakilisha nchi yetu katika Mashindano ya urembo ya Dunia ambayo kwa mwaka huo yalikuwa yafanyike barani Afrika nchini Nigeria lakini kutokana na sababu za kisiasa yalihamishiwa nchini Uingereza.
Mrembo Angela Damas baada ya kumaliza mwaka wake mmoja wa kazi za jamii, alifanya kazi katika Mashirika mbalimbali hapa nchini ikiwa ni pamoja na Kampuni ya simu za mkononi ya Mobitel [Buzz] kama Meneja Masoko. Kwa sasa mrembo Angela Damas yupo nje ya nchi akifanya kazi na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa. [UNDP]
2003: mrembo Sylivia Bahame kutoka Wilaya ya Temeke
2003: Warembo wa Jiji la D'salaam walikuwa wakibadilishana Taji la Miss Tanzania kutoka Wilaya ya Ilala mwaka 2002, Taji la Miss Tanzania 2003 lilinyakuliwa na mrembo Sylivia Bahame kutoka Wilaya ya Temeke. Na kama ilivyo ada mrembo Sylivia Bahame aliwakilisha nchi yetu katika Mashindano ya urembo ya dunia ambayo yalifanyika Sanya China .


Mrembo Sylivia Bahame aliyezaliwa tarehe 5 Juni 1983 baada ya kumaliza mwaka mmoja wa kazi za jamii, alirudi Chuo Kikuu cha D'salaam kuendelea na masomo yake ya Sheria, ambapo kwa sasa amemaliza na anafanya kazi kama Mwanasheria wa kujitegemea pia ameahidi kuwasaidia sana wanawake na wasichana warembo ambao watakuwa na matatizo mbalimbali.








                                                                   2004: mrembo Faraja Kotta kutoka Wilaya ya Kinondoni
Mwaka 2004 taji la Miss Tanzania lilihama kutoka Wilaya ya Temeke na kuchukuliwa na mrembo Faraja Kotta kutoka Wilaya ya Kinondoni. Mrembo Faraja Kotta aliweza kuonyesha kipaji chake tangu mwanzo aliponyakua taji la mrembo wa Kitongoji cha Ubungo, [Miss Ubungo] na baadaye kunyakua taji la Miss Kinondoni na hatimaye kuwa Miss Tanzania .


Faraja Kotta aliyezaliwa tarehe 6 Mei 1985 alikuwa na kila sababu ya kufurahia ushindi wake kwani ni katika kipindi hicho hicho alichoshinda taji la Miss Tanzania, alitangazwa kuwa Mwanafunzi bora wa kike wa mwaka 2004 kwa kuweza kushika nafasi ya juu, [Top 5] katika matokeo ya mtihani wa taifa wa kidato cha sita.
Mrembo Faraja Kotta aliwakilisha nchi yetu katika Mashindano ya urembo ya dunia ambayo kwa mara ya pili mfululizo yalifanyika tena Sanya nchini China . Mrembo Faraja Kotta baada ya kurejea nchini na kumaliza mwaka mmoja wa kazi za jamii alijiunga na Chuo Kikuu cha D'salaam ambapo anachukua masomo ya Sheria hadi hivi sasa.






                                                                         2005: Miss Tanzania Nancy Sumari
2005: Katika miaka 10 ya mwanzo ya Mashindano haya toka mwaka 1994 hadi 2004 yalikuwa yakiendeshwa kwa hasara huku Warembo wa Taifa wakijitahidi kufurukuta na kufanya vizuri ili kuibuka washindi katika Mashindano ya Urembo ya Dunia lakini waliambulia patupu hadi mwaka 2005 Miss Tanzania Nancy Sumari aliweka Historia ya Dunia kwa kunyakua Taji la Mrembo wa Dunia, Kanda ya Afrika. [Miss World Africa]


Ushindi ambao uliwafurahisha takribani Watanzania wote na kupokelewa na mapokezi makubwa yaliyoongozwa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, na baadaye kufanyiwa Tafrija kubwa ndani ya viwanja vya Ikulu.
Nyota ya Mrembo Nancy Sumari ilianza kung'ara tangu hapa Nchini baada ya kushinda Taji la Mrembo wa kitongoji cha Dar Indian Ocean mshindi wa pili nyuma ya mrembo Natalia Noel. Hata hivyo Mrembo Nancy Sumari hakukata tamaa alijifua zaidi na katika shindano la urembo la Kanda ya Kinondoni Mrembo Nancy Sumari aliweza kunyakua taji la Miss Kinondoni akimuacha mrembo Natalia Noel nyuma yake.


 
                                                                                        2006: WEMA SEPETU2006:
 Mrembo wa kwanza wa Taji la Vodacom Miss Tanzania , ni mrembo mwenye kipaji cha uigizaji na kwa sasa anavuma zaidi katika Filamu za Kitanzania.
 
 
                                                                                           2007: RICHA ADHIA
2007: RICHA ADHIA: Mrembo wa pili wa Taji la Vodacom Miss Tanzania , siku zote amekuwa mkereketwa wa kuanzisha Shule / Chuo cha masuala ya urembo, na kwa sasa amefungua Clinic yake ya masuala ya urembo ijulikanayo Beauty Clinic maeneo ya Mikocheni.
 
2008: NASREEN KARIM Mrembo
 
  2008: NASREEN KARIM Mrembo wa tatu wa Taji la Vodacom Miss Tanzania, ni mrembo aliyemaliza elimu ya Kidato cha 6 na kwa sasa anatarajia kujiunga na Chuo Kikuu kwa ajili ya masomo ya Juu









                                                                                              MREMBO 2009

2009: ILLUMINATA WIZE ,
Huyu ndiye mrembo ambaye taji la 
ulimbwende bado analishikilia na
kunako maajariwa atamkabidhi atakayeng'ara
miss Tanzania 2010.







                                     YAHUSUYO WAREMBO WA BONGO TZ


                                                                                (Toleo maalum la miss tz 2009 )
Tathmini ya miaka 15 ya shindano hilo, inaonesha kuwa kwa sasa asilimia kubwa ya Watanzania hawana kimuhemuhe na Miss Tanzania tofauti na angalau ilivyokuwa miaka minne iliyopita.


Katika hilo, Kamati ya Miss Tanzania inayoongozwa na Hashim Lundenga ‘Anko’, inalaumiwa kwa jinsi inavyowalea warembo na kuwaacha ni sawa na kondomu kwamba kazi yake ikiisha inatupwa na kutafutwa nyingine.
Mfano huo unachambuliwa kuwa Kamati ya Miss Tanzania mara inapompata mrembo na kumaliza kumtumia, humwacha akiwa hana A wala B mtaani, huku wao wakiangalia mtu mwingine atakayewawezesha kupata fedha mpya.
Mbele ya hilo, Kampuni ya Compass Communication inaonesha kuimarika zaidi katika shindano lake la Miss Universe kutokana na ushiriki wake mzuri kwenye fainali za dunia Miss Universe, pia jinsi inavyowatunza warembo wake.
Ijumaa Wikienda limegundua kuwa licha ya ukweli kuwa Miss Universe Tanzania ina miaka miwili tu tangu ianze mwaka 2007, lakini sera za Compass zimelenga kuwasaidia warembo.
Limebaini kuwa tangu mshindi wa mwaka juzi, Flaviana Matata mpaka wa mwaka huu, Illuminata Wise, Compass imeendelea kuwalea na kuwatafutia mikataba ya mitindo kwenye nchi mbalimbali, hivyo kuzidi kuboresha maisha yao.
Tofauti na Miss Universe ya miaka miwili, Miss Tanzania yenye miaka 15 mpaka leo hakuna mrembo inayoweza kujivunia kuwa imemtengenezea mazingira ya kuishi kama staa.
Ijumaa Wikienda lina ‘data’ za uhakika kuwa Kamati ya Miss Tanzania ipo kibiashara zaidi kwa kuwa inaangalia zaidi fedha za wazamini kuliko mrembo ambaye wanamvalisha taji kwa mwaka mzima.
Wajumbe wa kamati hiyo wanawekwa kizimbani na kusomewa mashtaka kwamba mara mrembo anaporudi kutoka Miss World, huwa hawana habari naye, isipokuwa hungoja kipindi kingine cha mavuno kutoka kwa wadhamini katika fainali zinazofuata.
Kufuatia tabia hiyo, hivi sasa kuna warembo wanahangaika mitaani, wakibaki kuwageuza mapedeshee kuwa mitaji yao kutokana na kukosa msingi bora Miss Tanzania.
Uchunguzi unaonesha kuwa shindano hilo huwapa umaarufu mkubwa warembo, hivyo hutaka kuishi kulingana na hadhi ya majina yao, kitu ambacho huwa ni kinyume baada ya kutelekezwa na kukosa msingi wa maisha.
Gazeti hili limebaini kuwa kutokana na kiu ya warembo kutaka kuishi maisha ya kifahari, huku Miss Tanzania ikiwa haijawapa dira, hujikuta wakigeuka watumwa wa ngono wa ‘mapedeshee’ ili tu waweze kupata ‘goodtime’.
Gazeti hili linakwenda mbali zaidi kwa kueleza kuwa mwaka 1994 wakati Aina Maeda anavalishwa taji la Miss Tanzania, mashindano hayo yalikuwa katika hali ya kusuasua.
Hata hivyo, mwaka 1998, wakati Basila Mwanukuzi anatawazwa Miss Tanzania, fainali hizo zilianza kuchangamka na kuwavutia zaidi Watanzania, kiasi cha kuwa gumzo la kitaifa kila fainali zilipowadia.
Tathmini inaonesha kuwa tangu mwaka 1997, shindano hilo limepoteza umaarufu na halina mvuto na kwamba mara ya mwisho watu kuhamasika na fainali hizo ni mwaka 2006, pale Wema Sepetu alipovalishwa taji.
Chanzo cha fainali hizo kupoteza umaarufu kinatajwa kuwa ni uteuzi wa warembo wabovu ambao wanashindwa kufanya lolote Miss World, pia kitendo cha Kamati ya Miss Tanzania kuyafanya mashindano hayo kuwa ya kitajiri.
Katika hilo, Kamati ya Miss Tanzania inalaumiwa na asilimia kubwa ya Watanzania kwa kutumia vibaya jina la nchi yao, wakati linawahusu wale wenye fedha nyingi peke yao.
Watanzania wanalaumu kuwa Kamati ya Miss Tanzania imeweka mbele tamaa ya pesa kwa kuweka kiingilio cha fainali hizo kuwa ni kati ya shilingi 50,000 na 100,000, kiasi ambacho ni kikubwa mno kwa Mtanzania wa kawaida.
Kamati ya Miss Tanzania, pia inalaumiwa kwa kuweka mbele ‘njaa’ kwa mdhamini kiasi cha kusahau wajibu wake wa kuandaa warembo wenye sifa.
Pointi nyingine inayotajwa kuondoa msisimko wa Miss Tanzania, ni kuporomoka kwa hadhi ya Miss Dar City Centre tangu mwaka 2004.
Kutokana na picha hiyo, watu mbalimbali wamekuwa wakitoa maoni kuwa pengine huu ndiyo mwanzo wa mwisho wa Miss Tanzania kwa kuwa katika macho ya sinema ni kama linakuwa kwa sababu ya wadhamini lakini kwenye mtazamo halisi linapumulia mashine.


Wema Sepetu kinara wa skendo Miss Tanzania
Miss Tanzania 2006-07, Wema Isaac Sepetu ndiye mrembo mwenye rekodi ya kuwa na skendo nyingi ambazo zilijulikana na kuandikwa na magazeti mbalimbali nchini.
Kwa mujibu wa tathmini ya warembo wote waliowahi kubeba taji la Miss Tanzania tangu mwaka 1994, Wema ndiye anayeongoza kwa skendo nyingi.
Skendo ya kwanza kuhusu mrembo huyo ni ile ya kushiriki mashindano ya urembo wakati akiwa na umri wa chini ya miaka 18, kitu ambacho ni kinyume cha taratibu za mashindano.
Habari ya kwanza kuhusu mrembo huyo kuwa ‘anda 18’, iliandikwa kwa mara ya kwanza na Ijumaa Wikienda, mwaka 2006 wakati Wema alipokuwa Warsaw Poland ambako Fainali za Miss World zilichukua nafasi.
Mara baada ya kurudi nchini akitokea Poland ambako alifanya vibaya, Wema alianza kuandamwa na skendo mbalimbali za ngono, rekodi ambayo haijavunjwa na waliomfuatia.
Katika skendo hizo, Wema alihusishwa kimapenzi na baadhi ya wafanyabiashara wenye majina makubwa Dar ambao hujulikana zaidi kama ‘mapedeshee’ kabla ya wasanii Khaleed Mohamed ‘TID’ na Heri Samir ‘Mr. Blu’ nao kutajwa kutoka naye.
Wema pia alitajwa kutoka na staa wa filamu, Steven Kanumba lakini wakawa wanakanusha kabla ya mambo yao kuwa kweupe ambapo baadaye waliachana kwa taadhira, ikiwemo kufikishana mahakamani.
Katika sakata hilo, Wema alilala mahabusu siku mbili kwenye Gereza la Segerea, Dar es Salaam akidaiwa kuvunja kioo cha gari la Kanumba.
Wema pia aliingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na mjasiriamali, Jumbe Yusuf Jumbe na kuzuka zogo kubwa la kifamilia ambapo mama wa Miss Tanzania huyo, Mariam Sepetu aliingilia kati.
Mss Tanzania huyo mstaafu pia anahusishwa kutoka na mbunge mmoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ingawa amekuwa akikanusha kwa nguvu zote.










Miss TZ yapongezwa


Baadhi ya wananchi waliohudhuria Fainali za Miss Tanzania mwaka huu wameimwagia sifa Kampuni ya Lino Internationl Agency Ltd na kamati nzima ya Miss Tanzania kwa kuonesha waziwazi kuwa inatenda haki.






Wananchi hao walinong’ona na gazeti hili kuwa kitendo cha majaji kumpa taji, Miriam Gerald anayetokea Mwanza, Kanda ya Ziwa kimeonesha kuwa hakuna upendeleo Miss Tanzania.






Walisema, fikra za wengi zilielekea kuwa kwa sababu mwaka jana, Nasreen Karim aliyetokea Mwanza, Kanda ya Ziwa kushinda, isingekuwa rahisi mtu wa kanda hiyo kuibuka tena mshindi.






“Hii imenipa hamasa na nimeamini Miss Tanzania ni wakweli, ingekuwa hawaangalii vigezo, hapa huyu dada wa leo asingeshinda, angetafutwa wa kutoka sehemu nyingine ili tu ionekane mshindi anaweza kutoka popote,” alisema Mark Kimodo wa Ubungo nje ya Ukumbi wa Mlimani City, Dar zilipofanyika fainali hizo.






Kamati ya Miss Tanzania imepongezwa kwa kutangaza utalii wa ndani kama ilivyo kauli mbiu ya mwaka huu ya mashindano hayo.






“Lundenga na wenzake wanastahili sifa, wamejitahidi kuutangaza utalii wa ndani, tunaomba waendelee hivi hivi,” alisema Rosemary Balinyukwa wa Kijitonyama, Dar kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini.






Richa Adhia ndiye miss kimeo?






Miss Tanzania 2007-08, Richa Adhia ameweka rekodi ya kuwa mrembo aliyeonekana kimeo tangu siku ya kwanza anakabidhiwa taji na aliendelea hivyo mpaka alipomaliza muda wake.






Richa, siku anakabidhiwa taji mwaka 2007 kwenye Viwanja vya Leaders, Kinondoni, Dar es Salaam umati mkubwa ulilipuka na kukataa matokeo hayo.






Hata hivyo, upo ukweli wa wazi kuwa sauti za Watanzania zilizopazwa, ziliongozwa na hali ya ubaguzi kwa sababu Richa ana asili ya Bara la Asia.






Tathmini inaonesha kuwa kukataliwa kwa Richa hakukuwa Miss Tanzania peke yake, kwani ‘nuksi’ ilimuandama mpaka Miss World baada ya Kamati ya Miss Tanzania kushindwa kumtumia DVD inayoonesha kazi za kijamii alizozifanya kabla hajaondoka.






Kwa matokeo hayo ya kutomtumia DVD, Richa alifanya vibaya Miss World na hata aliporudi alibaki kuwa mnyonge na kuweka rekodi ya kuwa mrembo mkimya zaidi Miss Tanzania.






Lundenga alivyoaibika kwa Nancy






Miss Tanzania 2005-06, Nancy Sumari ndiye mrembo aliyefanya vizuri zaidi na kutengeneza rekodi ambayo haijafikiwa na yeyote nchini kwenye Fainali za Miss World baada ya kufanikiwa kutinga Sita Bora na kubeba Taji la Miss World Africa.






Ushindi huo wa Nancy ulikuwa ni sawa na aibu kwa Mratibu wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga ambaye alimtabiria mrembo huyo kufanya vibaya hata kabla hajapanda jukwaani.






Nancy, mrembo aliyeingia Miss Tanzania akitokea Kanda ya Kinondoni, anabakiwa kuwa bora mpaka sasa kwani kabla yake hakuna mrembo nchini aliyefanya vizuri Miss World kumfikia na baada yake haijatokea.






























Mamisi vipenzi vya watu






Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu, 2000, Jacqueline Ntuyabaliwe, 2001, Happiness Magese, 2004, Faraja Kotta, 2005, Nancy Sumari, 2006, Wema Sepetu ndiyo warembo wenye mvuto zaidi kijamii.






Kwa mujibu wa tathmini ya gazeti hili, warembo hao ndiyo ambao wamebaki kwenye masikio na midomo ya Watanzania wengi.






Katika pointi hiyo, Miss Tanzania 2002, Angela Damas na wa 2003, Silvia Bahame wanakuwa warembo waliovutia zaidi wakati wakiwa na taji lakini baada ya kukabidhi wakazimika ghafla.






Hoyce, Jacqueline ‘K-Lynn’, Happiness, Faraja, Nancy na Wema wanashika rekodi ya kuwa na mvuto zaidi kwa sababu hawajasahaulika mpaka leo.






















Warembo waliodorora na mataji






Miss Tanzania 2007-08, Richa Adhia na wa 2008-09, Nasreen Karim ndiyo warembo ambao walipoteza mvuto wakiwa na mataji yao mkononi na kusababisha vipindi vyao kukosa mvuto na msisimko.






Hata hivyo, Nasreen aliwahi kulalamika kuwa anakosa ‘kampani’ kutoka Kamati ya Miss Tanzania ndiyo maana anashindwa kuchangamka na kufanya shughuli za kijamii.






Kwa upande wa Richa, ipo wazi kwamba aliathirika kisaikolojia tangu siku ya kwanza anakabidhiwa taji kwa kukataliwa na Watanzania na baadaye kukosa ushirikiano wa Kamati ya Miss Tanzania kwenye Fainali za Miss World, hivyo kumsababishia kufanya vibaya.[/left]
Source: ijumaa wikienda

No comments:

Post a Comment