KARIBUNI MCHICHANI

Kwa Habari moto moto Kuhusu Siasa , Uchumi, Maisha, Elimu Na Mengine Mengi.



Wednesday, September 22, 2010

Kijana avunja rekodi kwa uzazi holela UK

Macdonald
LONDON, Uingereza
KIJANA mwenye umri wa miaka 25, ameweka historia Uingereza kwa kuzaa watoto 15 na wanawake 14, na baadaye kuwatelekeza. Taarifa zilisema kijana huyo Keith Macdonald,

Monday, September 20, 2010

VUVUZELA LA KIBONGO NI KIBOKO YAO

Mkimbiza mwenge kitaifa ambaye anajulikana zaidi kwa jina la Masai kutoka mkoa wa Manyara akipuliza pembe la ng'ombe ambalo sauti yake vuvuzela la Afrika Kusini halioni ndani

Sunday, September 19, 2010

SHINDA MKOKO HUO HAPOOOOO!!!! , DUUU DUNIANI KUNA MAMBO

                           Kumbe duniani kuna magari yametengenezwa kwa kutumia majamvi. Hebu licheki hili Hammer.

                                                                                         Linavyoonekana kwa mbele

Shinda mkoko huo hapo kazi kwako

TUNAJIFUNZA NINI KUTOKA KWA BOB MARLEY AU KULA DUDE LA KIMATAIFA !!!!!! ????

                   

Bob Marley



Mcheza mpira wa miguu, Mhubiri wa amani na upendo, Mwanamapinduzi, Mwanaharakati, Mpiganaji, Mwanasiasa, Mwanamuziki wa Reggae na Nyota ya kwanza katika ulimwengu wa tatu Bob Marley.

Friday, September 17, 2010

NAKAAYA AIKACHA CHADEMA,AJIUNGA NA CCM!

Rafiki yangu mmoja aliwahi kuniambia jambo ambalo nilimbishia karibu mishipa ya fahamu initoke.Aliniambia kwamba vuguvugu lililopo nchini la vijana na hususani wasanii wa muziki wa kizazi kipya kujiunga na vyama vya siasa, linaongozwa na utashi wa kishabiki shabiki tu na pia tamaa ya fedha na kujiongezea tu umaarufu fulani katika jamii

HUYU HAPA HARD MAD

                                                                                      HARD MAD
Msanii wa muziki wa kizazi kipya HARD MAD jumapili hii anafanya video yake ya wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la AMKA UJITETEE chini ya production ya VISUAL LAB na mtayarishaji wake ni ADAM JUMA.

Tuesday, September 14, 2010

Mtanzania anayefuata nyayo za Oprah Winfrey

Tumezoea kuwaona watangazaji na waendesha vipindi vya televisheni maarufu kama vile Oprah Winfrey na kipindi chake Oprah Winfrey Show na Tyra Banks na kipindi chake The Tyra Banks Show wote hawa wakiwa ni wanawake wa Kiafrika wenye asili ya Marekani waliofanikiwa na kujizolea umaarufu kutokana na vipindi vyao hivyo.

Je, kuna ubakaji ndani ya ndoa?

Na John Ngunge

Suala la ubakaji kufanyika ndani ya ndoa kwa wanando au la, limekuwa linavuta hisia na kupewa mitazamo tofauti na watu tofauti. Makala hii yazungumzia baadhi watu mkoani Arusha wanavyolitazama suala hilo



Utekelezaji wa haki za binadamu katika maeneo ya kazi

Na Jackson Kimambo
14th September 2010

Kuna umuhimu wa kuzingatia haki za binadamu katika mazingira ya kazi ili kudumisha ufanisi hasa katika sekta binafsi na zile za umma ambapo waajiri na waajiriwa wanahitajika kupata elimu ya haki za binadamu mahali pa kazi kwa sababu kuna faida kubwa.

KURA ZA MAONI ZA CCM TARIME BADO NI MWIBA USIO NA TIBA

Wajumbe waangua kilio mkutanoni
Vidonda vya kura za maoni bado vinakiumiza Chama Cha Mapinduzi (CCM) jimbo la Tarime na juzi kikao cha usuluhishi na kuvunja kambi kilichokuwa kimeitishwa kiilisha bila kufikiwa kwa azma hiyo, baada ya baadhi ya wajumbe kuanza kuangua kilio wakiongozwa na mgombea aliyeangushwa akiamini alishinda kura hizo.

JUMBA LA BIG BROTHER - MAJI SHINGONI MWISHO NA KIMWANA CHA NAMIBIA, APUMUA KWA MASHINE.

Mshiriki wa shindano la Big Brother kutoka Tanzania, Mwisho Mwampamba akiwa an rafiki yake Uti kutoka Nigeria.
Mshiriki wa shindano la Big Brother kutoka Tanzania, Mwisho Mwampamba, amenusurika

Bilal apigwa butwaa

  • Mkutano wakosa watu, magari yakodishwa kuuokoa
  • Machungu yamzidi Mbega, Makamu UVCCM kusaidia
Fukuto la kura za maoni lingali linachemka ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kiasi cha kuathiri mahudhurio ya wanachama kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea Mweza, Dk. Mohammed Gharib Bilal, hali iliyolazimu kusafirisha watu kwa magari baada ya uwanja kuwa mtupu.

Monday, September 13, 2010

JK aendelea kufunika Tanga, amnadi Maji Marefu.

Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Stephen Ngonyani maarufu kama Profesa Majimarefu Mgombea ubunge Korogwe vijijini kwa tiketi ya CCM wakati

Dk.Slaa asema: Kumrudisha Kikwete ni kulizika taifa kaburini


MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amewataka Watanzania kutofanya makosa ya kumrejesha tena Ikulu, Rais Jakaya Kikwete. Slaa mgombea urais ambaye anaonekana kujenga ushawishi unaoonekana

JIONEE TABASAMU LA WAREMBO WA BONGO (SMILING FACES )

                                                            Geneveive Emmanuel Miss Tanzania 2010


Miss Tanzania 2010, Genevieve Emmanuel (katikati)akipunga mkono, akiwa na mshindi wa tatu, Consolata Lucas (kushoto) na mshindi wa pili Gloria Mwanga baada ya matokeo kutangazwa.  GENEVEIVE Emmanuel ambaye ni mtoto wa Meneja wa timu ya soka ya Yanga ya Dar es Salaam

Sunday, September 12, 2010

HAKI HUINUA TAIFA: WOSIA MWL.JK.NYERERE

BABA WA TAIFA ATAKUMBUKWA DAIMA

“Elimu yetu inatakiwa kutupa chanjo ya kujituma kwa ajili ya jamii nzima na kuwasaidia wanafunzi kukubali yale yanayokubalika kwa ajili ya maisha yetu ya mbeleni”. Baba wa Taifa, Mwl. J. K. Nyerere  “Elimu ni siraha ya nguvu kubwa unayoweza kutumia kuibadili dunia”. Nelson Mandela.  “Mizizi ya elimu ni michungu, lakini matunda yake ni matamu”. Aristotle.

Saturday, September 11, 2010

HISTORIA YA MIAKA 15 YA MISS TANZANIA.

                                                                              1994: Mrembo Aina Linda W. Maeda
Mara baada ya kushinda taji hilo na kumaliza mwaka wake mmoja wa kazi za jamii, alipata ofa mbalimbali za kufanya kazi za mitindo nchini Afrika ya Kusini, na hatimaye kuhamia huko na kuishi huko kwa karibu miaka 10 ambapo aliweza kupata marafiki wa jinsia mbalimbali na kutokana

HOMA YA KUMSAKA MISS YAANZA KUPAMBA MOTO, HIZI HAPA SURA ZA VISURA WA BONGO

Vipi KING MSWATI wa Swaziland akiwa kamisa wa miss Tanzania 2010 ???

MAMBO YA IDD HAYO

vipi ghafla kingetokea kimbunga hapo, duu heri mimi nikae mbali kidogo

FM ACADEMIA WAZINDUA "VUTA NIKUVUTE" KWA KISHINDO DIAMOND JUBILEE USIKU HUU!!

Mkurugenzi wa Mabibo Heineken Beer Benedicta Rugemalila kulia akipunga mikono mara baada ya kuizindua albama ya sita "Vuta Nikuvute" ya Bendi ya muziki wa dansi FM Academia kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee usiku huu akishirikiana kwa pamoja na Mkurugenzi wa Masoko wa Zain Kelvin Twisa wa pili kutoka kulia na Felician Mutta katikati, anayeonekana kuzungumza ni MC wa shughuli hiyo Benny Kinyaiya.

WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU NI JUKUMU LA NANI KUWALEA , KAMA SIYO WEWE NA MIMI ?


UMOJA wa watoto waishio katika mazingira hatarishi na magumu mitaani ujulikanao kama New Hope Family Street Children-NFSC, umewaomba wadau kujitokeza na kuwasaidia vitu mbalimbali ikiwemo magodoro, vitanda na vyombo vya ndani

Friday, September 10, 2010

RAY C KATIKA JITIHADA ZA KUUSAKA UREMBO NA USTAA


Akiwa msaani  machacha wa muziki binti wa kitanzania , aliwahi tajwa kuwa ni msaani mrembo zaidi afrika mashariki
Mambo ya sifa nyingi hayo, eti wahenga walisema sifa nyingi huharibu utamuu eeeeh !!??
Nataka niwe na wewe milele , kibao kilichogeuka kuwa kitanzi kwa Ray c, na kuwa sitaki kuwa na wewe milele , kwani watanionaje ?
Mcheza kwao hatuzwi, kujaribu na ugenini kukampelekea msaani huyo akipanda pipa  hadi  white house, huko akatamani lau angezaliwa Ulaya.


Lakini mwana wa kuku kamwe hatokuwa mwewe